1. Utangulizi
Sera hii ya Faragha inaeleza jinsi UTALIICHAT inavyokusanya, inavyotumia, na inavyolinda taarifa zako za kibinafsi unapochat na kutumia mfumo wetu. Tunaahidi kulinda faragha yako kwa mujibu wa sheria za ulinzi wa data.
2. Taarifa Tunazokusanya
Tunapokusanya taarifa zako, tunafanya hivyo ili kukupa huduma bora na za uhakika. Taarifa tunazokusanya ni pamoja na:
- Taarifa za Usajili: Jina lako, namba ya simu na barua pepe (email).
- Taarifa za Miamala: Namba za simu za M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money au Halopesa zinazotumika kupokea na kutoa malipo.
- Kumbukumbu za Kifaa: Data za mfumo (kama vile LocalStorage) kuhifadhi salio lako na historia ya jumbe ulizochat.
3. Jinsi Tunavyotumia Taarifa Zako
Taarifa zako zinatumika kwa madhumuni yafuatayo pekee:
- Kukamilisha miamala ya kutoa fedha (Withdrawals) papo hapo.
- Kuhakiki akaunti yako na kuzuia udanganyifu au akaunti za kughushi.
- Kukutumia taarifa muhimu za mfumo na fursa mpya za watalii kupitia WhatsApp.
4. Ulinzi na Usalama wa Data (SSL Encryption)
Jukwaa la UTALIICHAT linatumia teknolojia ya kisasa ya ulinzi ya 256-Bit SSL Encryption kuhakikisha taarifa zote zinazopita kwenye mfumo wetu ziko salama na hazijadukuliwa na mtu yeyote wa tatu.
5. Utoaji wa Taarifa kwa Watu wa Tatu
UTALIICHAT haitauza, haitakodisha, wala haitashiriki taarifa zako za kibinafsi kwa kampuni au watu wa nje, isipokuwa tu pale inapobidi kukamilisha miamala ya kifedha kupitia mitandao ya simu au inapotakiwa kisheria na mamlaka za serikali.
6. Haki Zako Kama Mtumiaji
Unayo haki ya kuomba kufutwa au kubadilishwa kwa taarifa zako za kibinafsi wakati wowote kwa kuwasiliana na timu yetu ya msaada kwa wateja.
7. Mabadiliko ya Sera Hii
Tunaweza kuboresha au kubadilisha sera hii mara kwa mara. Mabadiliko yoyote yakifanyika, yatapakiwa kwenye ukurasa huu mara moja.