UTALIICHAT
Teach Swahili • Earn Money
← Rudi Mwanzo

1. Utambulisho na Kukubali Masharti

Kwa kufungua, kutembelea, au kutumia jukwaa la UTALIICHAT, unakubaliana kikamilifu na vigezo na masharti yaliyoainishwa hapa. Ukawa haukubaliani na sehemu yoyote ya masharti haya, hauruhusiwi kuendelea kutumia huduma zetu.

2. Maelezo ya Huduma

UTALIICHAT ni jukwaa linalowaunganisha wazungumzaji wa Kiswahili na watalii pamoja na wanafunzi wa kimataifa wanaotaka kujifunza lugha na utamaduni wa East Africa. Jukwaa hili linatoa fursa kwa watumiaji kujipatia kipato kwa njia ya mazungumzo na mafunzo ya Kiswahili.

3. Usajili na Uamilisho wa Akaunti (Account Activation)

Ili kuanza kutumia huduma zote za mfumo na kuweza kutoa salio lako (Withdrawal) kwenda kwenye mtandao wako wa simu (M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money au Halopesa), lazima uwe na akaunti iliyothibitishwa na kuamilishwa.

4. Mfumo wa Malipo na Kutoa Pesa

Watumiaji wote wanapaswa kuzingatia miongozo ifuatayo kuhusu malipo:

5. Mwenendo na Maadili ya Mtumiaji

Watumiaji wote wa UTALIICHAT wanatakiwa kudumisha nidhamu na heshima ya hali ya juu wakati wa kuongea na watalii. Ni marufuku kabisa:

Mtu yeyote atakayekiuka miongozo hii akaunti yake itafungiwa mara moja bila taarifa wala kurudishiwa salio lake.

6. Mabadiliko ya Masharti

UTALIICHAT inahifadhi haki ya kubadilisha au kuboresha vigezo na masharti haya wakati wowote ili kukidhi mahitaji ya kisheria na maboresho ya huduma. Mabadiliko yakifanyika yatatangazwa kupitia ukurasa huu.

7. Msaada na Mawasiliano

Ikiwa una swali au changamoto yoyote kuhusu vigezo na masharti haya, unaweza kuwasiliana nasi kupitia Channel yetu rasmi ya WhatsApp au timu ya huduma kwa wateja.